Serikali haipo tayari kushuhudia mamia ya watanzania wakipoteza maisha –RPC MZINGA
JESHI la polisi mkoani Njombe limezuia mabasi mawili kuendelea na safari zake za mikoani na kulazimika kushusha abiria baada ya kubainika kuwa na ubovu wa kupindukia, huku madereva watatu wa mabasi hayo wakishikiliwa na jeshi hilo.
Hatua ya kusitisha safari za mabasi hayo imechukuliwa wakati wa operesheni ya ukaguzi wa magari ya abiria iliyofanywa na Jeshi la Polisi majira ya saa 12 asubuhi ikiwa na lengo la kutokomeza vifo vito kanavyo na ubovu wa vyombo vya moto pamoja na uzembe wa madereva .
Akizungumza na abiria wakati wa operesheni ya ukaguzi wa magari, Kamanda wa Polisi mkoa wa Njombe, Renata Mzinga alisema serikali haipo tayari kushuhudia mamia ya watanzania wakipoteza maisha kwa sababu ya ajali barabarani hivyo gari lolote litakalokutwa na dosari litasitishiwa safari mpaka pale litakapo rekebishwa.
Alisema kati ya madereva hao watatu, mmoja wao atafikishwa mahakamani kwa kukiri kuendesha basi la abiria likiwa bovu.‘’Dereva mmoja tutamfikisha mahakamani kwa kosa la kuendesha gari likiwa bovu, na akiwa na uhakika ni bovu,bado hata kwa magari madogo tutaendelea kukagua ni zoezi endelevu,” alisema Renata.
“Sheria zipo tutaendelea kuwashtaki kuendesha magari mabovu, tutasimamia sheria ili tuhakikishe vyombo vyote vinavyobeba abiria mkoani Njombe vipo salama,” alisema Renata.
Mbali na kusitisha safari za mabasi hayo Kamanda wa polisi pia alisema jeshi la polisi litamfikisha mahakamani dereva mmoja ambae amekutwa akisafirisha abiria ili hali basi lake ni bovu kupindukia.
Naye Mkuu wa kikosi cha Usalama wa Barabarani mkoa wa Njombe, Kelvin Ndimbo alisema wanaendesha oparesheni hiyo kukagua mabasi ya abiria kwa lengo la kuhakikisha abiria wanaotumia vyombo vya usafiri wanasafiri salama.
“Tunawategemea nyie madereva kila mara mmuendelee kufuata sheria za usalama barabarani na kuanzia tarehe 9 hadi 14 Julai tutatoa elimu bure ya usalama barabarani,” alisema Ndimbo.
Kufanyika kwa oparesheni hiyo mjini hapa jana ni mwendelezo wa Jeshi la Polisi nchini kupitia kikosi cha usalama barabarani kufanya ukaguzi wa magari kwa ajili ya kudhibiti ajali za barabarani zinazoendelea
kutokea.
Mtaa wa Lunyanywi
Postal Address: P.O.Box 668-Njombe
Telephone: 026 278 291 213
Mobile:
Email: ras@njombe.go.tz
Copyright ©2019 GWF . All rights reserved.