Shirika la Hifadhi ya Jamii (NSSF) limetoa Msaada wa Mabati Elfu moja (1000) kwa ajili ya kukamilisha ujenzi wa Vituo vya Afya na Shule za msingi na Sekondari katika wilaya ya Makete.
Akikabidhi Msaada huo kwa Mbunge wa jimbo la Makete ,Kaimu Mkurugenzi wa Uendeshaji shirika hilo Bathlow Mmuni amesema lengo la kutoa msaada huo ni kurudisha kiasi cha faida wanayoipata kwa jamii na wataendelea katika sekta mbalimbali.
Akipokea msaada huo Mbunge wa jimbo la Makete Profesa Norman Sigalla amesema msaaada huo utasaidia kukamilisha majengo ya zahanati na shule ambayo wananchi Wameshajenga kwa hatua ya kuta pia ametoa wito kwa mashirika mengine kuisaidiaa wilaya hiyo kwani bado inakabiliwa na changamoto mbalimbali.
Naye Mkuu wa wilaya ya Makete Bi .Veronica Kessy ametoa wito kwa wananchi wa Wilaya hiyo kuendelea kujenga Zahanati kila kijiji kwani kufanya hivyo itawasidia kusogeza huduma za afya karibu.
Wananchi walioshuhudia makabidhiano hayo wameshukuru Shirika la Hifadhi ya Jamii (NSSF) kwa kutoa msaada huo.
Mtaa wa Lunyanywi
Postal Address: P.O.Box 668-Njombe
Telephone: 026 278 291 213
Mobile:
Email: ras@njombe.go.tz
Copyright ©2019 GWF . All rights reserved.