Mkuu wa mkoa wa NJOMBE CHRISTOPHER OLE SENDEKA ameatoa wito kwa jamii ya Mkoa wa Njombe kuwa na desturi ya kuwapeleka watoto kufanya tohara ili kupunguza maambukizi ya Ukimwi mkoani hapa.
Akiongea katika mkutano wa wadau wa Afya Mkoa wa Njombe OLE SENDEKA amesema kuwa swala la ugonjwa wa ukimwi linatakiwa kusemwa wazi na kuelemisha vijanaa na jamii bila kificho.
Takwimu zinzonyesha mkoa wa Njombe umeendelea kuwa kinara kwa maambukizi kwa asilimia 14.8 ukifuatiwa na mikoa ya Iringa wenye asilimia 9.1 na Mbeya wenye 9.0 hatua ambayo imeilazimu serikali kwa kushirikiana na shirika lisilo la serikali JPAIGO kuona umuhimu wa kuingiza mradi wa SAUTI ili kutoa elimu juu ya maambukizi , upimaji afya pamoja na uhamasishaji wa Tohara kwa wakazi wa mkoa Njombe
Baadhi ya wajumbe wa Mkutano huo wanaomba wadau kuendelea kushirikiana na Serikali kutoa elimu kwa jamii ili kupunguza maambukizi mapya
meneja mwandamizi wa Mradi wa SAUTI TAIFA NELSON LUTABANZIBWA anasema kutokana na maambukizi kuwa juu katika mkoa wa Njombe shirika la JPAIGO Kupitia mradi wa SAUTI limeanza kutoa elimu kuhusu ugonjwa wa ukimwi, huduma za tohara pamoja na upimaji afya
Mtaa wa Lunyanywi
Postal Address: P.O.Box 668-Njombe
Telephone: 026 278 291 213
Mobile:
Email: ras@njombe.go.tz
Copyright ©2019 GWF . All rights reserved.