• Complaint |
    • Contact Us |
    • FAQ |
    • Staff Mail |
MKOA WA NJOMBE

The United Republic of Tanzania President's Office Regional Administration and Local Government MKOA WA NJOMBE

  • Home
  • About Us
    • Historical Background
    • Mission and Vision
    • Core Values
  • Administration
    • Organization Structure
    • Sections
      • Administration & HR Section
      • Local Government Section
      • Planning & Coordination Section
      • Economic & Production Section
      • Infrastructure Section
      • Education Section
      • Health Section
    • Units
      • Finance & Accounts Unit
      • Internal Audit Unit
      • ICT Unit
      • Procurement & Supply Unit
      • Legal Unit
  • District
    • Njombe District
    • Wanging'ombe District
    • Makete District
    • Ludewa District
  • Councils
    • Njombe TC
    • Njombe DC
    • Wanging'ombe DC
    • Makete DC
    • Ludewa DC
    • Makambako Tc
  • Investment Opportunities
    • Agriculture
      • Crop production
      • Livestock
      • Fisheries
      • Forestry
    • Tourism
    • Mining
  • Services
    • Health Services
    • Education Services
    • ICT Services
    • Infrastructure Services
    • Water Services
  • Publications
    • Guidelines
    • Procedures
    • Reports
    • Laws
    • Forms
    • Strategic plan
    • Client Service Charter
  • Media Center

Naibu waziri wa maji na umwagiliaji Nchini Jumaa Aweso ametangaza kiama kwa watakaobainika kula fedha za mradi wa maji .

Posted on: October 6th, 2018

Naibu waziri wa maji na umwagiliaji Nchini Jumaa Aweso ametangaza kiama kwa watakaobainika kula fedha za mradi wa maji kijiji cha ukarawa halmashauri ya wilaya ya Njombe mkoani Njombe na kwamba watazitapika.

Aweso alitoa kauli hiyo jana katika ziara yake ya siku nne Mkoani Njombe ambapo akiwa wilayani Njombe akizungumza na wananchi wa kijiji cha ukarawa mara baada ya kukagua mradi wa maji ambao serikali imeshamlipa mkandarasi milioni 530 katika mradi huo ambao umekamilika wenye thamani ya zaidi ya milioni 560 lakini wananchi bado wanakabiliwa na adha ya kupata maji unaotarajiwa kuhudumia wakazi wa vijiji vya ukarawa na itole .

‘’Mradi huu ni wa miaka mingi wakati mwengine mnasababisha mama zetu wanashindwa kupaka mafuta wala poda kutokana na kukosekana kwa maji’’aliongeza Aweso.

Mhandisi wa maji hamashauri ya wilaya ya Njombe Rajab Yahaya alimueleza naibu waziri juu ya matumizi ya fedha ambapo milioni 10 hazijulikani zilipo.

‘’mradi huu niliukuta umeanza na kwamba hadi sasa mkandarasi amelipwa milioni 532 na kiasi kilichobaki ni shilingi milioni 20 ndio zipo katika akaunti na hizo milioni 10 haijulikani ilipo ’’alisema Yahaya.

Naibu waziri huyo alisema kuwa lazime ifike hatua watu waogope fedha za miradi ya maji.


‘’wakati mwengine mambo hayawezi kwenda sawa,lazima ifike hatua tusioneane haya..haiwezekani miaka yote maji hakuna na fedha tayari zimeshalipwa’’alisema

Mara baada ya kukagua mradi huo Naibu Waziri Aweso anagundua matumizi mabaya ya fedha za kuendeshea mradi huo na kwamba ameagiza kuitwa kwa aliyekuwa mhandisi na mkandarasi wa mradi wa maji wa kijiji cha ukarawa halmashauri ya wilaya ya Njombe ili kuja kutolea maelezo ya sintofahamu ya fedha kiasi cha shilingi Milioni Kumi ambazo hazijulikani zilipo.

‘’jambo la msingi tunapotoa milioni 562 tulitegemea wannachi hawa wapate maji..tunavituo zaidi ya 13 napata taarifa kitole hakuna hata kituo kimoja kinachotoa maji sasa mimi ninachokuomba mhandisi wa maji wewe huwezi kuachiwa maradi lazima umeachiwa na fedha…na nikuagize mhandisi ambaye alikuwa anasimamia mradi huu Johakim Sanga mpigie simu aje aasubuhi kwa mkuu wa mkoa na lazima nichukue hatua

Maelezo hayo hayakumridhisha Naibu Waziri aweso anatoa agizo la kutafutwa kwa aliyekuwa mhandisi wa mradi huo joakim kinganola sanga pamoja na mkandarasi wake kihanga farm and transportation ili kuja kutolea ufafanuzi zaidi.

Kwa upande wake mbunge wa jimbo la Lupembe Joram Hongoli alisema mradi huo umechukua muda mrefu bila mafanikio.

‘’mbaya zaidi katika kijiji cha kitole mpaka hatua hii hakuna ata tone moja la lililotoka’’alisema Hongoli.

 

Christopher philemon

Afisa habari mkoa wa njombe

0715 717042

Announcements

  • WANAFUNZI WALIOCHAGULIWA KUJIUNGA NA KIDATO CHA KWANZA 2024MKOA WA NJOMBE January 08, 2024
  • TAARIFA KWA UMMA May 10, 2023
  • TAARIFA YA UHAMISHO OFISI YA MKUU WA MKOA WA NJOMBE October 14, 2023
  • View All

Latest News

  • DR. MICHAEL HAULE WA NM-AIST AMTEMBELEA MKUU WA MKOA WA NJOMBE.

    June 25, 2025
  • MWEKEZAJI NEIL GOODTILLERE WA BROWNS PLANTATION AKUTANA NA MKUU WA MKOA WA NJOMBE.

    June 25, 2025
  • MAFUNZO MAALUMU KWA MADEREVA WA TAASISI ZA SERIKALI YAENDELEA MKOANI NJOMBE.

    June 14, 2025
  • MKUU WA MKOA WA NJOMBE MHE. ANTHONY MTAKA ASHIRIKI IBADA YA KUAGA MWILI WA MZEE MONGELLA JIJINI DAR ES SALAAM.

    June 04, 2025
  • View All

Video

Music
More Videos

Quick Links

  • Vivutio vya Utalii mkoani Njombe
  • Fursa za kilimo cha matunda aina ya maparachichi
  • MATOKEO YA KIDATO CHA NNE 2024/2025
  • Maktaba ya Picha
  • Maktaba ya Video

Related Links

  • Tovuti ya Temesa
  • Tovuti ya Tanroads
  • Tovuti ya Wizara ya Ujenzi

World visitors tracker

world map hits counter

Visitors Counter

writingMasterThesis

Location Map

Contact Us

    Mtaa wa Lunyanywi

    Postal Address: P.O.Box 668-Njombe

    Telephone: 026 278 291 213

    Mobile:

    Email: ras@njombe.go.tz

Other Contacts

   

    • Privacy Policy
    • Disclamer
    • FAQ
    • Sitemap
    • Service

Copyright ©2019 GWF . All rights reserved.