MKUU wa mkoa waNjombe Christopher Ole Sendeka amemuagiza mkurugenzi wa halmashauri ya Wilayaya Wanging’ombe Bi .Amina Kiwanuka kuhamisha fedha milioni mia 300 zilizopelekwakatika zahanati ya Palangawanu kupelekwa katika kituo cha afya cha Wanging’ombemara moja kwaajili ya ukarabati wa kituo hicho.
Sendekaalifikia uamuzi huo mara baada ya kubaini mchezo mchafu uliofanywa na baadhi yaviongozi na kusababisha mkanganyiko wa fedha hizo ambazo zilikuwa kiasi chashilingi milioni mia 4 na kuahidi kuwachukulia hatua bila kujali ni kina nanikwa kuwa bila kufanya hivyo yeye atafukuzwa kazi.
“Mpangowa ukarabati wa zahanati hizo siyo mradi uliyoibuliwa na wananchi wala madiwanibali ni mradi wa serikali kuu hivyo kitendo cha kubadilisha fedha na kuziletakatika zahanati ya Palangawanu ni makosa makubwa na kitendo hiki siwezikukifumbia macho,” alisema.
Alisemaserikali kupitia Ofisi ya rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (TAMISEMI) iliamuakukarabati vituo vya afya mia moja nchi nzima ili kuboresha huduma ya afya hasakwa upande wa upasuaji ndipo walipotenga fedha kwaajili ya kazi hiyo nazahanati ya Wanging’ombe mkoani Njombe ilifanikiwa kuingia katika mchakato huo.
Aliongezakuwa baada ya kukamilika kwa mchakato huo fedha za awamu ya kwanza kiasi chashilingi milioni mia 4 zilitolewa kwaajili ya kituo cha Wanging’ombe lakinikuna baadhi ya viongozi walienda kuwalaghai maafisa wa TAMISEMI na kuwatakakuzituma fedha hizo katika kituo cha afya cha Palangawanu.
“Kituohiki hakina sifa ya kupata fedha hizo kwa kuwa ni zahanati ila kwasababu yaushawishi waliokuwa nao watu hao walifanikiwa kuwalaghai maafisa wa TAMISEMI nakuzipeleka fedha hizo kusikotakiwa na ahidi kuwachukulia hatua kali za kisheriawatu hao pindi nitakapowabaini,” alisema.
Aidhaalibainisha kuwa fedha hizo mara baada ya kufika katika zahanati hiyo zilianza kazina baada ya wiki moja mchezo huo ulibainika na zoezi la ujenzi wa zahanati hiyoulisitishwa mpaka suala hilo litakapo zungumzwa na kuwekwa sawa.
Mpakajana mkuu wa mkoa ana muamuru mkurugenzi wa halmashauri ya Wilaya yaWanging’ombe kurudisha fedha hizo kwenye akaunti ya kituo cha afya chaWanging’ombe tayari kiasi cha shilingi milioni mia moja zilishatolewa na kiasicha shilingi milioni 32 zimeshatumika na milioni 28 ni madeni ambayo wanatakiwakulipa watu wanaowadai.
Kufuatiahali hiyo Sendeka aliwataka kuchukua kiasi hicho cha shilingi milioni mia mojana kuhakikisha wanakarabati zahanati ya Palangawanu mpaka ikamilike kwakushirikiana na wananchina kiasi cha shilingi milioni mia 3 zilizobakikuzipeleka katika akaunti ya kituo cha afya cha Wanging’ombe.
Wakatihuo huo aliwataka wanasiasa wanaoendesha siasa za maji taka na kuwashauriwananchi kuacha kuchangia miradi ya maendeleo kuacha siasa hizo mara moja nakuahidi kuwashughulikia.
“Wanasiasawanaoendesha siasa za maji taka nitashuka na nyie vinginevyo mjirekebisheharaka,” alisema
Kwaupande wake diwani wa kata ya Wanging’ombe Geofrey Nyagawa alisema januari mosi2018 ni siku ambayo wananchi wa Wanging’ombe walichukia mno mara baada yakusikia fedh hizo zimepelekwa Palangawanu lakini Februari 8 ni siku ambayowamefurahi kupata haki yao ya msingi mara baada ya mkuu wa mkoa kumuamurumkurugenzi kufanya hivyo mara moja kabla ya februari 10 .
Nayekatibu mkuu kiongozi mstaafu Philemoni Luhanjo alimpongeza mkuu wa mkoa waNjombe kwa kusimamia mkoa vizuri na kutoa maamuzi ya haki kwa wananchi wake.
“Siyosahihi viongozi kuwahujumu wananchi wao kwa kuwa wao ndiyo wasimamizi wa hakiza wanachi wao wanapokuwa mstari wa mbele kuipoteza haki wanapoteza imani kwawatu wanaowaongoza,” alisema.
MWISHO
Mtaa wa Lunyanywi
Postal Address: P.O.Box 668-Njombe
Telephone: 026 278 291 213
Mobile:
Email: ras@njombe.go.tz
Copyright ©2019 GWF . All rights reserved.