FURSA ZA UWEKEZAJI, MAENEO YALIYOTENGWA, CHANGAMOTO NA MIKAKATI UWEKEZAJI MKOA WA NJOMBE HADI JUNI, 2019
A. FURSA ZA UWEKEZAJI ZILIZOPO KATIKA MKOA
Mkoa una fursa nyingi za kuwekeza, kuanzisha viwanda na shughuli za kibishara kutokana na hali nzuri ya hewa, wakulima waliobobea, umeme na maji ya uhakika. Fursa hizi zinaweza kutumiwa na Wawekezaji mbalinawake wajasiriamali kuwekeza ili kiunua kipato chao na kukuza uchumi. Baadhi ya fursa zilizopo ni pamoja na:-
1. Kuongeza Thamani Mazao ya Kilimo, Mbogamboga na Matunda
a. Viwanda vya uchakataji mazao ya kilimo na kuongeza thamani kwenye mazao ya Chai, Pareto, Alizeti (Double Refining), Mpunga, Mbogamboga, Viazi Mviringo na Kahawa katika halmashauri zote
b. Kusindika Matunda na Mboga Mboga – Parachichi, Nyanya, Mananasi na Matofaa (Apples) pamoja na kilimo cha Maua katika Halmashauri za Ludewa, Makete, Njombe na Makambako Mji
2. Kuongeza Thamani Mazao ya Misitu na Maliasili
b. Uchakataji wa Mazao ya Misitu – Ukataji wa Magogo, Nguzo, Mbao, Play Wood, Hard Board na mazao mengine ya misitu pamoja na utengenezaji wa Mkaa kwa kutumia mabaki ya vumbi la mbao.
c. Ufugaji na uchakataji mazao ya nyuki katika halmashauri zote.
d. Uvuvi wa kisasa wa samaki wa kula katika halmashauri zote na samaki wa mapambo katika ziwa Nyasa wilaya ya Ludewa.
3. Kuongeza Thamani Mazao ya Mifugo
Usindikaji wa vyakula vya mifugo, Machinjio za kisasa, Viwanda vya maziwa na Utotoleshaji wa vifaranga Bora vya Kuku.
4. Nishati na Madini
a. Uchimbaji wa Chuma na Makaa ya Mawe katika Wilaya za Ludewa na Makete.
b. Uwekezaji katika umeme wa maji katika maporomoko ya Itipula kwenye mto Ruhuji, Wilaya ya Njombe, Ketawaka katika mto Ketawaka katika Wilaya ya Ludewa, Mto Mlomboji katika Wilaya ya Wanging’ombe, na Maporomoko ya Lumakali Katika Wilaya ya Makete.
c. Uchimbaji wa shaba Nyeusi katika Wilaya za Ludewa, Njombe na Makete. Pamoja na uchimbaji mdogo wa madini na dhahabu, Green Tormarine, Blue Sulphur na Rose Garnet katika Halmashauri za Ludewa, Makete, Njombe (W) na Njimbe Mji.
d. Ujenzi wa mitambo ya umeme wa Upepo katika Halmashauri za Wanging’ombe, Njombe na Makambako
5. Utalii, huduma za Hoteli na Ukarimu
a. Ujenzi wa mahoteli ya Kitalii katika fukwe za ziwa Nyasa kwenye vijiji vya Lupingu, Manda na Makonde katika Wilaya ya Ludewa.
b Ujenzi wa Hoteli za kitalii ndani ya hifadhi ya Taifa ya Kitulo iliyopo Wilaya ya Makete na Pori la Akiba la Mpanga Kipengere katika Wilaya ya Wanging’ombe kwenye mwambao wa fukwe za ziwa Nyasa.
c. Utalii wa kutembea katika safu za milima ya Living Stone na Ukenju wilaya ya Ludewa.
d. Huduma za kutembeza watalii katika vivutio vya utalii.
6. Viwanda vinginevyo, Maghala na miundombinu mingine
a. Viwanda vya maji ya kunywa.
b. Utengenezaji wa vifungashio mbadala.
c. Utengenzaji wa Chaki.
d. Ujenzi wa Bandari Kavu Makambako.
e. Ujenzi wa Majengo ya Kibiashara Njombe (Business Complex Malls).
f. Ujenzi wa Maghala na viwanda vya Unga Wilaya za Njombe na Ludewa
B. MAENEO YALIYOTENGWA KWA AJILI YA UWEKEZAJI NKOA WA NJOMBE
a) Halmashauri ya Mji Njombe
NA |
KATA |
ENEO LA VIWANDA LILILOTENGWA(EKARI) |
MAENEO YALIYOLIPWA FIDIA (EKARI) |
MAENEO YALIYOPIMWA (EKARI) |
MAENEO YENYE HATI MILIKI
|
MAELEZO MENGINE |
1 |
Kifanya
|
Ujenzi wa Kiwanda cha Chai - Unilever Tanzania Ltd (Ekari 20)
|
EKARI 20
|
EKARI 20
|
Eneo hili (Ekari 20) limepimwa na kumilikishwa kwa mwekezaji kupitia ‘National Land Allocation Committee’ na mwekezaji Unilever Tanzania Ltd. ( Ameandaliwa Derivative Right kwa mujibu wa sheria).
|
Mwekezaji ameanza kazi.
|
3 |
Uwemba
|
Ujenzi wa Chuo cha VETA Kijiji cha Magoda
|
|
Ekari 30
|
Eneo limepimwa, Fidia bado haijalipwa.
|
|
4 |
Njombe Mjini
|
Eneo kwa ajili ya Kukusanyia na kuhifadhia Matunda na Mboga mboga (Sorting, Grading and Parking) kabla ya kupelekwa kwenye masoko- Ekari 10.12 (mita za mraba 39,916)
|
Ekari 10.12
|
Ekari 10.12
|
Eneo limepimwa na Hati itatolewa baada ya mazungumzo kati ya TAHA na Halmashauri kukamilika
|
|
6 |
Kifanya
|
Eneo kwa ajili ya ujenzi wa Kiwanda cha Mbao (Timber Processing Industry)- Ekari 130.
|
Bado
|
Ekari 130
|
Eneo limepimwa, bado halijamilikishwa na halijapata mwekezaji. Eneo lina miundombinu ya Barabara, Maji na Umeme ipo- Halijalipiwa fidia
|
Matangazo yamewekwa kwenye tovuti ya halmashauri ili kuvutia wawekezaji
|
7 |
Ramadhan
|
Ujenzi wa Soko la Kisasa kwa ajili ya Viazi mviringo (Ekari 3)
|
Halijalipiwa fidia
|
Ekari 3
|
Limepimwa bado hati haijatolewa
|
Halijapata wawekezaji
|
8 |
Utalingolo
|
Ujenzi wa Kituo cha kuchambua na kupanga kwenye madaraja Viazi mviringo –Utalingolo (Ekari 20)
|
Halidaiwi fidia ni eneo la serikali
|
Ekari 20
|
Limepimwa na hati bado haijaandaliwa
|
Halmashauri imeomba fedha Wizara ya fedha na mipango ili kuwekeza katika mradi huo
|
9 |
Uwemba
|
Ujenzi wa Viwanda mbalimbali
|
|
Ekari 50
|
Limepimwa na hati bado haijaandaliwa
|
|
|
|
|
|
|
|
|
b) Halmashauri ya Wilaya ya Njombe
Maeneo ya Wafanyabiashara
Eneo lenye ukubwa wa Ekari 13.25 linamilikiwa na wananchi wa kijiji cha Mtwango limetengwa kwenye mchoro wa Mipango Miji Na. 52/01/1208 kwa ajili ya wafanyabiashara, viwanda vidogo. Tayari kuna miundombinu ya umeme, maji na barabara. Eneo litapimwa kwa kuwashirikisha wananchi.
Ekari 21.74 zinamilikiwa na kijiji cha Ilunda kwa ajili ya ujenzi wa mnada, mafunzo ya wanayamakazi pamoja na soko la mbao. Eneo hilo limepimwa na tayari kuna miundombinu ya umeme, maji na barabara na linatarajiwa kundelezwa kwa matumizi.
Maeneo ya wajasiriamali
Hekta 6010 zimetengwa kupitia mradi wa SAGCOT kwenye kata za Ikondo (2350), Mfriga (23,50), Mtwango (65), Igongo lo (20) na Idamba (1225) kwa ajili ya shughuli za misitu, kilimo na viwanda vidogo. Maeneo hayo yanamilikiwa na Halmashauri za vijiji na yanatarajia kupimwa na kuendelezwa
Eneo lenye ukubwa wa ekari 15 katika kijiji cha Matembwe linalomilikiwa na kikundi cha UWAMIMA limetengwa kwa ajili ya soko la mbao. Enelo limepimwa na lina miundombinu ya umeme, maji na barabara, linatarajiwa kuendelezwa kwa matumizi husika.
Maeneo ya Uwekezaji
Eneo lenye ukubwa wa ekari 5.32 linamilikiwa na Halmashauri ya Wilaya ya Njombe kwenye kiwanja Na. 165/D limetengwa kwa ajili ya kujenga majengo ya vitega uchumi (Njombe Business Complex). Eneo limepimwa na kuna miundombinu ya umeme, maji na barabara. Linatarajiwa kuendelezwa kwa matumizi husika.
Viwanja 12 (Na.85-96/D) vyenye nyumba 25 zinazomilikiwa na Halmashauri ya Wilaya ya Njombe katika Mtaa wa National Housing kutajengwa majengo ya vitega uchumi kwa ajili ya kupangisha. Viwanja hivyo vimepimwa na tayari kuna miundombinu ya umeme, maji na barabara. Viwanja vitaendelezwa mwaka wa fedha 2019/20.
c) Halmashauri ya Wilaya ya Wanging’ombe
Halmashauri imefanikiwa kutenga jumla ya maeneo 361 Kwa matumizi ya viwanja vya biashara, maeneo 86 kwa matumizi ya viwanda vidogo katika kata 18 na maeneo makubwa 12 ambayo yameainishwa kwa ajili ya uwekezaji katika jedwali lifuatalo.
Mahali lilipo (Kata/Kijiji) |
Ukubwa (Ekari) |
Kama limepimwa (mipangomiji) kama halijapimwa litapimwa lini |
Umiliki wake (linamilikiwa na nani) Halmashauri au Taasisi/mtu binafsi |
Shughuli inayopendekezwa kufanyika hapo (limetengwa kwa ajili ya viwanda gani, kilimo cha nini) |
Miundombinu (barabara, maji, umeme) ambayo tayari imeshawekwa |
Mipango kazi ya uendelezaji wa eneno lililopo (ioneshe tarehe ya mwisho wa utekelezaji) |
Bajeti iliyotengwa kwa shughuli ya uendelezaji 2018/2019 |
Kata ya Mdandu – kijiji cha Mdandu
|
20 |
Bado halijapimwa, upimaji utafanyika kupitia bajeti ya mapato ya ndani
|
Maeneo yanahitaji kutwaliwa na kulipwa fidia
|
Eneo la viwanda kwa ajili ya utengenezaji wa bidhaa zitokanazo na matunda (parachichi na tikiti maji)
|
Umeme upo kijijini
Maji yapo |
Uendelezaji wake unategemea upatikanaji wa wawekezaji
|
Hakuna
|
Kata ya Mdandu – kijiji cha Ihanja
|
24 |
Bado halijapimwa, upimaji utafanyika kupitia bajeti ya mapato ya ndani
|
Maeneo yanahitaji kutwaliwa na kulipwa fidia
|
Eneo la viwanda kwa ajili ya uchakataji wa mazao ya misitu
|
Umeme haupo
Maji yapo |
Uendelezaji wake unategemea upatikanaji wa wawekezaji
|
Hakuna
|
Kata ya Usuka – kijiji cha Usuka
|
20 |
Bado halijapimwa, upimaji utafanyika kupitia bajeti ya mapato ya ndani
|
Maeneo yanahitaji kutwaliwa na kulipwa fidia
|
Eneo la uzalishaji wa mazao ya asali
|
Umeme upo kijijini
Hakuna maji |
Uendelezaji wake unategemea upatikanaji wa wawekezaji
|
Hakuna
|
Kata ya Imalinyi – kijiji cha Imalinyi
|
25 |
Bado halijapimwa, upimaji utafanyika kupitia bajeti ya mapato ya ndani
|
Maeneo yanahitaji kutwaliwa na kulipwa fidia
|
Eneo la utengenezaji wa bidhaa zitokanazo na nyama pamoja na maziwa
|
Umeme upo kijijini
Maji yapo |
Uendelezaji wake unategemea upatikanaji wa wawekezaji
|
Hakuna
|
Kata ya Kidugala – kijiji cha Masaulwa
|
10 |
Bado halijapimwa, upimaji utafanyika kupitia bajeti ya mapato ya ndani
|
Maeneo yanahitaji kutwaliwa na kulipwa fidia
|
Eneo la uzalishaji wa mazao ya asali
|
Umeme haupo
Maji yapo |
Uendelezaji wake unategemea upatikanaji wa wawekezaji
|
Hakuna
|
Kata ya Wanging’ombe – kijiji cha Mung’elenge
|
45 |
Bado halijapimwa, upimaji utafanyika kupitia bajeti ya mapato ya ndani
|
Maeneo yanahitaji kutwaliwa na kulipwa fidia
|
Eneo la uanzishwaji wa viwanda kwa ajili ya kuzalisha bidhaa za kilimo
|
Umeme haupo
Maji yapo |
Uendelezaji wake unategemea upatikanaji wa wawekezaji
|
Hakuna
|
Kata ya Wanging’ombe – kijiji cha Kijombe
|
75 |
Bado halijapimwa, upimaji utafanyika kupitia bajeti ya mapato ya ndani
|
Maeneo yanahitaji kutwaliwa na kulipwa fidia
|
Eneo la uanzishwaji wa Ranchi kwa ajili ya uzalishaji wa nyama na mazao ya ngozi na maziwa
|
Umeme haupo
Maji hakuna |
Uendelezaji wake unategemea upatikanaji wa wawekezaji
|
Hakuna
|
Kata ya Ilembula – kijiji cha Igula
|
10 |
Bado halijapimwa, upimaji utafanyika kupitia bajeti ya mapato ya ndani
|
Maeneo yanahitaji kutwaliwa na kulipwa fidia
|
Eneo la viwanda kwa ajili ya kuongeza thamani mazao ya nafaka (mahindi, karanga na alizeti)
|
Umeme upo kijijini
Maji yapo |
Uendelezaji wake unategemea upatikanaji wa wawekezaji
|
Hakuna
|
Kata ya Luduga – kijiji cha Luduga
|
20 |
Bado halijapimwa, upimaji utafanyika kupitia bajeti ya mapato ya ndani
|
Maeneo yanahitaji kutwaliwa na kulipwa fidia
|
Ufugaji wa kuku na nyuki pamoja na uzalishaji wa mazao ya nyuki
|
Umeme upo kijijini
Maji yapo |
Uendelezaji wake unategemea upatikanaji wa wawekezaji
|
Hakuna
|
Kata ya Luduga – kijiji cha Mambegu
|
10 |
Bado halijapimwa, upimaji utafanyika kupitia bajeti ya mapato ya ndani kwa mwaka ….
|
Maeneo yanahitaji kutwaliwa na kulipwa fidia
|
Ufugaji wa nyuki na uzalishaji wa mazao ya nyuki
|
Umeme upo kijijini
Maji yapo |
Uendelezaji wake unategemea upatikanaji wa wawekezaji
|
Hakuna
|
Kata ya Luduga – kijiji cha Iyayi
|
16 |
Bado halijapimwa, upimaji utafanyika kupitia bajeti ya mapato ya ndani kwa mwaka ….
|
Maeneo yanahitaji kutwaliwa na kulipwa fidia
|
Ufugaji wa kuku na nyuki pamoja na uzalishaji wa mazao ya nyuki
|
Umeme upo kijijini
Hakuna maji |
Uendelezaji wake unategemea upatikanaji wa wawekezaji
|
Hakuna
|
|
|
|
|
|
|
|
|
d) Halmashauri ya Wilaya ya Makete
Maeneo ya Uwekezaji na Shughuli za Vijana
Na |
Mahali Lilipo |
Ukubwa(Ha) |
Limepimwa |
Umiliki |
Shughuli |
Miundo Mbinu |
Mipango Kazi |
Bajeti Iliyotengwa |
1 |
Mfumbi
|
250 |
√ |
Jamii
|
Kilimo na mboga
|
Barabara,umeme,mifereji ya umwagiliaji
|
x |
x |
2 |
Ikuwo
|
128 |
√ |
Jamii
|
Kilimo cha maharage,parachichi na mahindi
|
Barabara
|
x |
x |
3 |
Matamba
|
200 |
x |
Jamii
|
Kilimo cha Viazi,pareto na parachichi
|
Barabara,umeme,maji
|
x |
x |
4 |
Luwumbu,bulongwa, na kipagalo
|
120 |
√ |
Jamii
|
Kilimo cha apple,maharage,mboga,parachichi na pareto
|
Barabara
|
x |
x |
5 |
Ipelele na Iniho
|
50 |
x |
Jamii
|
Kilimo cha maharage,apple,mboga,parachichi na pareto
|
Barabara
|
x |
x |
6 |
Iwawa, Kitulo na Isapulano
|
100 |
x |
Jamii
|
Kilimo cha matufaa,viazi na pareto
|
Barabara na umeme
|
x |
x |
7 |
Tandala na Lupalilo
|
80 |
x |
Jamii
|
Kilimo cha maharage,parachichi,apple na mboga
|
Barabara na Umeme
|
x |
x |
8 |
Ipepo na Ukwama
|
100 |
x |
Jamii
|
Maharage,parachichi na mahindi
|
Barabara
|
x |
x |
9 |
Mang’oto na Mbalatse
|
200 |
x |
Jamii
|
Apple,viazi na pareto
|
Barabara
|
x |
x |
10 |
Iwawa
|
256.25 |
X |
Jamii/ Umma
|
Huduma za jamii, biashara na Viwanda vidogo
|
Barabara
|
x |
x |
11 |
Tandala
|
161.87 |
X |
Jamii/ Umma
|
Huduma za jamii, biashara na Viwanda vidogo
|
Barabara
|
x |
x |
e) Halmashauri ya Mji Makambako
Na |
HALMASHAURI |
ENEO TENGWA |
UKUBWA |
MAONI |
1. |
Mji Makambako |
Kilimahewa |
Ekari 154.4 |
Soko la Kimataifa |
Ekari 15 |
Viwanda |
|||
Makambako |
Mita za mraba 96.6 |
Viwanda na fidia imelipwa |
||
Kiumba |
Ekari 4.2 |
Wajasiriamali na fidia tayari |
||
|
|
Mtwele |
Ekari 86.4 |
Uwekezaji wa umeme wa upepo |
|
|
Kivavi |
Ekari 18.3 |
Uwekezaji wa umeme wa upepo |
|
|
Kifumbe |
Ekari 102.6 |
Uwekezaji wa umeme wa upepo |
f) Halmashauri ya Wilaya ya Ludewa
NA |
ENEO |
AINA YA RASILIMALI |
JINA LA MWEKEZAJI |
UKUBWA WA ARDHI (ekari) |
MMILIKI |
1 |
Nkomang’ombe
|
Makaa ya mawe
|
NDC Co Chine’s Company
|
1900 |
Shirika la Maendeleo ya Taifa (NDC)
|
2 |
Ketewaka
|
Makaa ya mawe
|
Maganga Matitu
|
9683 |
Maganga Matitu Kampuni (MMRDL)
|
3 |
Kimelembe
|
Eneo la ujenzi wa viwanda
|
Maganga Matitu
|
251 |
Maganga Matitu (MMRDL)
|
4 |
Muhumbi
|
Shaba na dhahabu
|
Tumaini mining Cooperative Co Dewji and Partners Company
|
1316 |
Chama cha Ushirika cha Tumaini
|
5 |
Lifua
|
Ardhi ya kilimo cha mpunga
|
Kikundi cha kilelevana
|
350 |
Kikundi cha Wajasiliamali Kilelavanu
|
6 |
Mlangali
|
Msitu wa mbao
|
Halmashauri ya wilaya
|
150 |
Halmashauri ya wilaya
|
Msitu wa mbao
|
Wabia wanatafutwa
|
1,689 |
Sekta Binafsi
|
||
7 |
Ludende
|
Msitu wa mbao
|
Halamshauri ya wilaya
|
96 |
Halmashauri ya wilaya
|
Msitu wa mbao
|
Wabia wanatafutwa
|
309 |
Sekta Binafsi
|
||
8 |
Madope
|
Msitu wa mbao
|
Halmasharui ya wilaya
|
152 |
Halmashauri ya wilaya
|
Msitu wa mbao
|
Wabia wanatafutwa
|
856 |
Sekta Binafsi
|
||
9 |
Amani
|
Ujenzi wa viwanda
|
M.M.I
|
563 |
Maganga Matitu Kampuni (MMRDL)
|
10 |
Mundindi
|
Uchimbaji wa chuma
|
NDC CO Chinese Company
|
6621 |
Shirika la Maendeleo ya Taifa (NDC)
|
11 |
Amani
|
Uchimbaji dhahabu
|
Kabenge and partiners mineral Company
|
119 |
Kampuni ya Kaberege na Wabia
|
12 |
Njelela
|
Ardhi ya upandaji miti
|
Halmashauri ya wilaya
|
103 |
Halmashauri ya wilaya
|
13 |
Ilininda
|
Ardhi ya upandaji miti
|
Halmashauri ya wilaya
|
56 |
Halmashauri ya wilaya
|
14 |
Manda
|
Kilimo cha mpunga
|
Halmashauri ya wilaya
|
1404 |
Halmashauri ya wilaya
|
15 |
Ibumi (Masimavalafu)
|
Kilimo cha mpunga
|
Halmashauri ya wilaya
|
950 |
Halmashauri ya wilaya
|
16 |
Ludewa Mjini
|
Ujenzi wa viwanda
|
EPZ (Eneo limetengwa)
|
1500 |
EPZ
|
17 |
Ludewa Mjini
|
Ujenzi wa viwanda vidogo na vya kati
|
Wajasiliamali wadogo na wakati
|
464 |
Wajasiliamali wadogo na wakati
|
18 |
Ludewa Mjini
|
Ujenzi wa viwanda na maeneo ya Biashara
|
Halmashauri ya wilaya
|
300 |
Halmashauri ya wilaya
|
|
|
|
|
|
|
C. CHANGAMOTO KATIKA KUVUTIA UWEKEZAJI NA KUENDELEZA VIWANDA
a) HALMASHAURI YA MJI NJOMBE
a. Fidia ya Ardhi hasa kwa maeneo ya Mjini na Wananchi kutoridhia maeneo yao kutumika kwa shughuli za viwanda.
b. Miundombinu hafifu;
c. baadhi ya maeneo yaliyotengwa hayana barabara Imara, maji wala umeme.
d. Baadhi ya viwanda havina barabara imara, maji na umeme mfano Kiwanda cha maji -Nole hakina umeme hivyo wanatumia jenereta.
e. Mitaji midogo na gharama za uzalishaji kuwa kubwa hivyo kupelekea uzalishaji kuwa chini ya malengo na kupata faida ndogo.
f. Ujuzi mdogo wa wataalamu na ushindani usio sawa unaotokana na bidhaa bandia na zile zinazoingia pasipo kufuata taratibu
g. Ukosekanaji wa masoko na maghala.
h. Baadhi ya viwanda vinakabiliwa na changamoto ya udogo wa eneo mfano kiwanda cha Tenende kinachozalisha sembe
b) Halmashauri ya Wilaya ya Njombe
Kukosekana kwa umeme kwenye baadhi ya maeneo ambayo wawekezaji wameonesha nia ya kwekeza
c) Halmashauri ya Wilaya ya Wanging’ombe
Changamoto kubwa ni kuwa maeneo pendekezwa hayajatengwa na kupimwa kwa kufuata sheria, taratibu na kanuni, hivyo inatakiwa kuhakikisha kuwa zinapatikana fedha kwa ajili ya upimaji wa maeneo mbalimbali ya uwekezaji yaliyotengwa na kulipa fidia kwa wenye maeneo ili yawe huru kwa umilikishaji na hatimaye uendelezaji wake.
d) Halmashauri ya Wilaya ya Makete
Maeneo mengi ya uwekezaji yametengwa ila bado kulipwa fidia ili uwekezaji uanze kufanyika
Ukosefu wa miundombinu ya maji, umeme na barabara katika maeneo ya uwekezaji
Ukosefu wa nguvu kazi kwani vijana wengi wenye nguvu wamekuwa wakihama Makete
e) Halmashauri ya Mji Makambako
Ukosefu wa fedha kulipa fidia maeneo yanayotengweqa kwa ajili ya uwekezaji.
Kupanda kwa thamani ya ardhi
Baadhi ya wawekezaji waliochukua maeneo kwa uwekezaji kutoanza shughuli kwa wakati
Kuchewesha kulipwa fidia wananchi katika mradi wa Soko la Kimataifa Makambako
f) Halmashauri ya Wilaya ya Ludewa
Ukosefu wa fedha kulipa fidia maeneo yanayotengwa kwa ajili ya uwekezaji.
D. MIKAKATI YA KUENDELEZA VIWANDA NA UWEKEZAJI
a) Halmashauri ya Mji Njombe
a. Kuendelea kutenga maeneo kwa ajili ya viwanda na masoko.
b. Kutafuta masoko ya bidhaa nje ya Mkoa na Nchi.
c. Kuendelea kuboresha miundombinu ya barabara, umemena maji ili kurahisisha /kupunguza gharama za uzalishaji hususani katika kusafirisha malighafi na bidhaa.
d. Kuendelea kutoa mikopo kupitia Vikundi vya wanawake na vijana ili kuwaongezea mitaji.
e. Kuendelea kutoa elimu ya ujasiriamali katika jamii hii itasaidia kuboresha uzalishaji na jamii iweze kuibua viwanda vingine vipya.
b) Halmashauri ya Wilaya ya Njombe
a. Kuendelea kutenga maeneo kwa ajili ya viwanda na masoko.
b. Kutumia Mradi wa Umeme vijijini awamu ya tatu kupata umeme kwenye vijiji vingi zaidi
c) Halmashauri ya Wilaya ya Wanging’ombe
Kuendelea kutenga maeneo kwa ajili ya Uwekezaji
d) Halmashauri ya Wilaya ya Makete
Kuendelea kutenga maeneo kwa ajili ya Uwekezaji
e) Halmashauri ya Mji Makambako
Kuendelea kutenga maeneo kwa ajili ya Uwekezaji.
Kuendelea kuweka miundombinu ya maji, umeme na barabara kwenye maeneo ya uwekezaji
Kushawishi wakezaji wa ndani na nje kuwekeza katika Halmashauri
f) Halmashauri ya Wilaya ya Ludewa
a. Kuboresha kiwanda cha kuchakata kahawa katika kata ya mawengi.
b. Kununua mashine ya kubangua korosho ambayo itafanya kazi katika kata ya Luilo na Masasi.
c. Kununua mtambo wa kukoboa na kusaga mahindi na kufungasha unga katika kata ya Mavanga.
d. Kutoa elimu kwa wamiliki wa viwanda vidogo vidogo ili waweze kuviboresha zaidi na kuvikuza hatiamae vikawa viwanda vya kati.
Mtaa wa Lunyanywi
Postal Address: P.O.Box 668-Njombe
Telephone: 026 278 291 213
Mobile:
Email: ras@njombe.go.tz
Copyright ©2019 GWF . All rights reserved.