Mkoa una eneo la kilomita za mraba 24,994 sawa na hekta 2,499,400 ambapo eneo linalofaa kwa kilimo ni hekta 1,090,000 sawa na asilimia 43.6. Katika eneo hilo eneo lililolimwa kwa msimu 2017/18 ni hekta 368,530 sawa na asilimia 34 ya eneo linalofaa kwa kilimo.
Mkoa umepata mafanikio ya sekta hii katika maeneo ya upatikanaji wa chakula, kuongeza uzalishaji wa mazao ya biashara, na upatikanaji wa mbolea.
Kwa msimu wa kilimo wa mwaka 2017/18, Mkoa umezalisha tani 602,362 za mazao ya nafaka na tani 766,003 za viazi mviringo, viazi vitamu, ndizi na mhogo pamoja na tani 54,473 za mikunde na kufanya jumla ya tani 1,422,838.
Hivyo, kiasi halisi cha chakula kitakachopatikana kwa msimu wa 2018/19 kuwa tani 855,143 (Nafaka tani 602,362 na tani 252,781 ya viazi mviringo, viazi vitamu, ndizi na mhogo baada ya kuondoa maganda, na tani 54,473 za Mikunde).
Kwa mwaka, Mkoa unahitaji tani 173,621 za chakula ambapo chakula kilichopatikana (msimu 2017/18) ni tani 855,143, hivyo Mkoa ulikuwa na ziada ya tani 681,522 za chakula kama ilivyooneshwa kwenye kiambatisho Na. 2.
Mazao ya biashara yanayolimwa ndani ya Mkoa ni pamoja na Chai, Pareto, Maua, Alizeti, Kahawa, Ufuta, Korosho, Miwa, Matunda ya aina mbali mbali, Shayiri na Karanga. Kwa mwaka 2017/18 tani 86,964 za mazao ya biashara zilivunwa kutoka eneo la ukubwa wa heka 37,471 kama inavyooneshwa kwenye jedwali Na. 37.
Jedwali Na. 37: Uzalishaji wa Mazao ya Biashara kwa msimu wa mwaka 2017/18
Na |
Zao |
Hekta zilizolimwa |
Tani zilizovunwa |
|
Alizeti
|
13,216 |
12,243 |
|
Pareto
|
1,388 |
1,094 |
|
Kahawa
|
149 |
564 |
|
Chai
|
8149 |
42,071 |
|
Korosho
|
10 |
8 |
|
Matunda
|
8,385 |
21,270 |
|
Miwa
|
138 |
2,735 |
|
Maua
|
2 |
2 |
|
Ufuta
|
322 |
379 |
|
Karanga
|
5,142 |
6,597 |
|
Jumla
|
37,471 |
86,964 |
Uzalishaji wa Parachichi
Zao la Parachichi limeanza kupata umaarufu mkubwa kuanzia msimu wa 2016/2017 ambapo makampuni ya ndani na nje ya Nchi yalionesha nia ya kununua zao hilo. Katika msimu wa mwaka 2017/2018 jumla ya hekta 1,597 zilipandwa parachichi aidha, uzalishaji ulifikia tani 3,211 na kati ya hizo tani 38.3 zilinunuliwa na makampuni Makampuni ya Lima Kwanza Tanzania Ltd na Tanzanice yaliyosafirisha Parachichi hizo nchi za Ubelgiji, Uholanzi, na Uingereza. Makampuni mengine yaliyonunua parachichi ni pamoja na KUZA AFRICA COMPANY LTD, KEITT, Simba Logistic Equipment Supply. Wakulima waliuza kwa bei ya wastani kati ya shilingi 1000 hadi 1,500 kwa kilo moja.
Kampuni ya Alvardo imeanza maandalizi ya kujenga kiwanda cha kusindika parachichi katika halmashauri ya Wanging’ombe.
Kutokana na mafanikio haya makubwa (upatikanaji wa soko na Ujenzi wa kiwanda), Mkoa umejipanga kushirikiana nawadau mbalimbali kuendelea kutoa elimu kwa wakulima na jamii kwa ujumla ili kuwezesha uzalishaji wa parachichi za kutosha zenye ubora unaokidhi mahitaji ya soko.
Mkoa una mbolea ya kutosha kwa matumizi ya wakulima kwa musimu wote wa kilimo. Bei elekezi ya Serikali inatumika kwa mbolea za DAP na UREA, hali hii imesaidia kutopanda kwa bei kiholela na kuwafanya wakulima wengi kumudu kuinunua.
Mtaa wa Lunyanywi
Postal Address: P.O.Box 668-Njombe
Telephone: 026 278 291 213
Mobile:
Email: ras@njombe.go.tz
Copyright ©2019 GWF . All rights reserved.